- 9,516 viewsDuration: 4:46Katika muda wa majuma kadhaa yaliyopita, Rais William Ruto amejipata katika njia panda, akilazimika kuingilia kati baada ya misukosuko kuibuka katika sekta mbalimbali hapa nchini. Ni hapo jana tu ambapo Ikulu ya Rais ililazimika kutoa mwelekeo kuhusu mgogoro kuhusu raia wa kigeni haswa raia wa Burundi uliotokana na matamshi yake wiki iliyopita. Haya yanajiri huku Rais pia akilazimika kutatua malumbano kati ya mamlaka ya ushuru nchini KRA na wafanyabiashara wadogo. Sam Gituku anaangazia matatizo ambayo yamekumba afisi za mawasiliano serikalini katika siku za hivi punde