- 5,364 viewsDuration: 2:50Rais William Ruto ameendelea na ziara yake maeneo ya kusini mwa Bonde la Ufa, akisisitiza kuwa ametekeleza ahadi alizowapa Wakenya tangu alipochukua usukani mwaka 2022. Akiwahutubia wakazi wa kaunti za Kericho na Bomet, Rais Ruto amewahimiza watu wa jamii za eneo hilo kujitokeza kwa wingi kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa Agosti mwaka ujao, akisema analenga kupata zaidi ya kura milioni nne katika ngome yake.