- 2,157 viewsDuration: 3:20Rais William Ruto sasa anasema kuwa aliruhusu ujenzi wa kituo cha karantini cha Ebola katika kambi ya kijeshi ya Laikipia ili kuisaidia Kenya kupambana na virusi vya ugonjwa huo. Akizungumza huko Wajir wakati wa mahojiano na wanahabari wa Kaskazini mwa Kenya, Ruto amesema kuwa yeye ndiye aliyeruhusu mpango huo na kuwasuta wanasiasa kwa kuingilia swala hilo. Rais anasema kituo hicho kitasaidia kuwakinga Wakenya dhidi ya ugonjwa wa Ebola.