- 3,757 viewsDuration: 1:07Rais William Ruto ameendelea kutetea hatua yake ya kusitisha oparesheni za kiwanda cha madini cha Tata Chemicals eneo la Magadi, kaunti ya Kajiado. Rais amesema hatua hiyo inalenga kuhakikisha hakuna mali ghafi inayotolewa nchini bila kuongezewa thamani, akitaka viwanda vya humu nchini kuimarisha uzalishaji na kuongeza thamani ya bidhaa. Rais Ruto ameyasema hayo leo katika kaunti ya Samburu, kama anavyotuarifu Boniface Barasa.