- 4,032 viewsDuration: 3:26Rais William Ruto ametetea mipango ya serikali yake akiwashutumu wapinzani wanaopinga safari zake za mara kwa mara, akiwataja kama waliokosa uzalendo na wanaoendeleza siasa za kupinga maendeleo. Akizungumza katika kongamano la 11 kuhusu bahari huko Mombasa, Rais Ruto amesema upinzani umekosa sera na kusisitiza kuwa safari zake zimeendelea kuzaa matunda kupitia mikutano ya kimataifa iliyoandaliwa nchini katika kipindi cha miaka mitatu ya utawala wake. Na kama anavyoarifu Francis Mtalaki, serikali imeahidi kuongeza uwekezaji katika sekta ya uchumi wa majini.