- 3,482 viewsDuration: 2:53Rais William Ruto ametetea ujenzi wa Ikulu ndogo katika msitu wa Imenti kaunti ya Meru, akiwakosoa wanaopinga mradi huo kwa kile alichosema ni kupinga maendeleo ya eneo hilo. Kauli ya Rais Ruto imejiri baada ya Mahakama ya Mazingira eneo hilo kusitisha ujenzi huo ambao unapendekezwa kujumuisha anga tua pamoja na uwanja wa gofu. Akizungumza Meru leo, Rais Ruto pia aliwashambulia wapinzani wake wa kisiasa akisema ana imani ya kuibuka mshindi katika uchaguzi mkuu wa urais wa mwaka ujao.