- 2,418 viewsDuration: 3:00Rais William Ruto amewapongeza wakazi wa Nairobi kwa kudumisha amani wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu za Juni 25. Hata hivyo, Rais hakusita kuwasuta viongozi wa upinzani kwa kile alichosema ni kuhimiza maandamano ya vurugu. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa barabara ya daraja la juu ya Ngong’ Road–Naivasha Road, Rais alisifia ushirikiano kati ya serikali yake na ile ya Kaunti ya Nairobi akisema umechangia mageuzi ya maendeleo jijini. Emmanuel Too ana mengi zaidi.