Skip to main content
Skip to main content

Ruto: Malalamishi ya ardhi Lamu yatatatuliwa kwa haki

  • | Citizen TV
    4,003 views
    Duration: 3:04
    Rais William Ruto amesema malalamishi ya wakazi wa Lamu kuhusu zaidi ya ekari 7,000 za ardhi yatasikilizwa na kutatuliwa kwa haki. Ruto amesema wakazi hao watakuwa mstari wa mbele kunufaika na mradi wa ujenzi wa kiwanda cha kusafisha mafuta ghafi katika kaunti hiyo. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo, mwekezaji Aliko Dangote amesema kiwanda hicho chenye thamani ya Sh2.2 trilioni kitakamilika ndani ya miaka mitatu na kutoa ajira 60,000 kwa Wakenya.