- 3,735 viewsDuration: 2:47Rais William Ruto amesema serikali itatwaa asilimia 90 ya ardhi iliyokuwa ikimilikiwa na Tata Chemicals huko Kajiado, baada ya kuagiza kampuni hiyo ifungwe. Ruto amesema ardhi hiyo itarejeshewa wakazi wa Kajiado, huku kandarasi ya kampuni hiyo ikitangazwa upya ili kuvutia wawekezaji zaidi. Aidha, Rais amesema hakuna kampuni itakayoruhusiwa kumiliki zaidi ya ekari 30 za ardhi Kajiado.