Mswada unaolenga kuasisi sheria ya kwanza kuhusu teknolojia ya uzazi wa kisayansi sasa upo kwenye meza ya Bunge la Seneti baada ya kuidhinishwa na Bunge la Kitaifa. Lakini hata kabla ya mswada huo kujadiliwa, tetesi zimeibuliwa kuhusu njama ya kurejesha vipengee tata vilivyoondolewa na Bunge la Kitaifa. Shinikizo hilo linalotoka kwa baadhi ya madaktari, mawakala na wasambazaji vifaa, litawaathiri pakubwa kina mama wanaobeba mimba, watoto wanaozaliwa kwa njia hii na kliniki zinazotoa huduma za uzazi wa kisayansi, iwapo Seneti itashawishika.