- 1,621 viewsDuration: 2:41Kwa miezi kadhaa sasa, wahuni wameendelea kuvuruga amani na kuvamia mikutano ya kisiasa, shughuli zao zikisababisha maafa, majeraha na uharibifu wa mali, huku asasi za serikali za kiusalama zikishindwa kukabiliana nao. Licha ya ahadi ya Rais William Ruto na Waziri wake wa Usalama Kithure Murkomen, zogo hilo la wahuni limeendelea kusambaa bila kusitishwa, likisalia kuwa ahadi tu. Je, serikali imeshindwa kukabiliana na wahuni hao? Emmanuel Too ana mengi kwenye taarifa ifuatayo.