- 1,319 viewsDuration: 1:13Serikali imewahakikishia Wakenya kuwa imejipanga kikamilifu kukabiliana na mvua za El Niño zinazotarajiwa kunyesha katika msimu ujao wa mvua za vuli, huku hatua mbalimbali zikiwa tayari zimewekwa ili kupunguza madhara yanayoweza kutokea. Akizungumza katika eneo bunge la Manyatta, Kaunti ya Embu, Waziri wa Utumishi wa Umma Geoffrey Ruku amesema serikali imetenga rasilimali za kutosha kushughulikia dharura zozote zitakazoweza kusababishwa na El Niño.