katibu wa wizara ya ulinzi wa jamii Joseph Motari amesema serikali inaweka mikakati ya kuhakikisha watu wenye ulemavu wanahusishwa kikamilifu katika masuala ya maendeleo bila ubaguzi. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mfumo wa kimkakati wa kuongoza ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu katika maendeleo kwa kipindi cha mwaka 2026 hadi 2030, Motari alihimiza serikali za kaunti, mashirika yasiyo ya kiserikali, taasisi za elimu na sekta binafsi kushirikiana na serikali kuu ili kuhakikisha utekelezaji wenye mafanikio wa mfumo huo.