- 188 viewsDuration: 2:08Msukumo wa kuratibu ubora wa kitaaluma barani Afrika umeongezeka huku Mamlaka ya Kitaifa ya ubora wa kitaaluma ya Kenya yaandaa kwa mara ya kwanza kongamano la kitaifa la siku tatu linalolenga kuimarisha utambuzi wa masomo na uhamaji wa ujuzi nchini na barani Afrika kwa ujumla. Kongamano hilo linaangazia ulinganifu wa mifumo ya sifa za ubora wa kitaaluma ili kuhakikisha kwamba vyeti vinavyopatikana katika nchi moja vinatambuliwa kote barani. Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Katibu wa Idara ya mafunzo ya ufundi Esther Muoria asema kuwa mfumo huo utawawezesha wanafunzi kuendelea na masomo kwa urahisi kutoka vyeti vya msingi hadi kiwango cha shahada ya uzamifu.