Skip to main content
Skip to main content

Serikali yapuuza madai ya zabuni JKIA, yatoa ufafanuzi wa gharama

  • | Citizen TV
    2,767 views
    Duration: 3:34
    Serikali imepuuzilia mbali madai kuwa mfanyabiashara kutoka Zimbabwe amepokezwa zabuni ya upanuzi wa uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta International Airport. Waziri wa Uchukuzi Davis Chirchir amesema kuwa ripoti kwamba mfanyabiashara huyo amepewa zabuni ya mabilioni ya pesa ni za kupotosha, akieleza kuwa waliowasilisha maombi wametaja majina yote ya washirika wao wa kibiashara. Aidha amesema mpango huo utaiigharimu serikali angalau shilingi bilioni 154 na si mabilioni yanayotajwa.