- 1,423 viewsDuration: 3:42Serikali sasa inasema idadi ya watu waliokwama kwenya jumba lililoporomoka mtaani South C ni wawili na wala si wanne. Waziri wa utumishi wa umma na mipango maalum Geoffrey Ruku amesema uchunguzi uliofanywa kwa kukagua kanda za CCTV umethibitisha kuwa ni watu wawili pekee waliokuwemo wakati wa tukio na ambao bado hawajapatikana. Ruku amesema uchunguzi unaendelea na wote waliohusika na utepetevu watachukuliwa hatua. Mmoja wa wamiliki wa jengo hilo amejisalimisha kwa polisi