- 12,252 viewsDuration: 2:26Hatua ya Rais William Ruto kuifunga kampuni ya kemikali ya Tata Chemicals huko Magadi imeibua hisia miongoni mwa viongozi wa upinzani. Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna amemkosoa Rais, akisema hatua hiyo inalenga kuwatia hofu na kuwafurusha wawekezaji nchini, huku akiitaja kuwa ukiukaji wa sheria. Viongozi wengine wa upinzani pia wamemsuta Rais, wakimtuhumu kuhujumu uhuru wa wananchi na wanahabari.