Mabadiliko ya hali ya anga huendelea kuleta changamoto mbalimbali za kiafya huku misimu tofauti ikihusishwa na ongezeko la baadhi ya magonjwa.
Katika msimu huu wa baridi, matatizo ya mzio maarufu kama allergies yameripotiwa kuongezeka, huku watu wenye magonjwa nyemelezi wakionekana kuwa miongoni mwa walio katika hatari zaidi.
Katika siha na maumbile hii leo, Dakta Dominic Osiemo wa kituo cha Equity Afya Nairobi West anaeleza aina mbalimbali za matatizo ya afya yanayokithiri kipindi cha baridi na mbinu za kujikinga na kukabiliana nayo.
Taarifa zaidi zinafuata.