Skip to main content
Skip to main content

Tafakari Ya Babu: Harusi ya Kinubi

  • | Citizen TV
    607 views
    Duration: 1:06
    Tafakari ya Babu Juzi kwa siku mbili kulikuwa na harusi ya ndovu kumla mwanawe… kosa uchekwe! Katika nikah ya mwandani wangu wa dhati, Ali Noor na Amina Ramata, kulikuwa na wapambe wa kutosha, nami nikawa msaidizi wa bwana harusi. Ilikuwa ni nikah iliyokutanisha tamaduni mbili—Kinubi na Kiborana. Muda mfupi kabla ya harusi, ikaongezeka tamaduni ya Kisudan. Bwana harusi na msaidizi wake tukapakwa hina… si ile hina unayoijua ya Kiswahili, hii ilipakwa mikono yote, mbele na nyuma! (onyesha mikono). Mwisho wa siku, watu wakala, wakanywa kwa kefu yao, kisha wakasakata doluka hadi usiku. Yatafakari hayo.