- 2,704 viewsDuration: 59sBabu yangu hufuatilia kwa karibu sana siasa za Kenya na za kimataifa. Alipoona yaliyotokea Ol Kalou, alinipigia simu. Baada ya kuzungumza kwa muda, akaniambia: "Unajua porini kuna wanyama wengi, lakini wote humuogopa simba." Nikamsikiliza. Akaendelea: "Ni ushujaa mkubwa ukifaulu kumfukuza simba hadi akakimbia. Kwa kuwa ndiye anayeogopwa zaidi, ukimfukuza utajihisi bingwa. Lakini ni hatari sana kufuata nyayo zake. Hujui mbele alipoenda atapinduka lini, wala atarejea kwa namna gani." Nilibaki nikiyatafakari maneno ya babu. Na wewe, yatafakari.