Skip to main content
Skip to main content

Tahadhari yatolewa kuhusu ongezeko la dawa bandia sokoni

  • | Citizen TV
    2,865 views
    Duration: 2:55
    Wataalamu wa afya wameibua tahadhari kuhusu ongezeko la dawa bandia sokoni, hususan dawa za kutibu Virusi vya Ukimwi, dawa za matatizo ya nguvu za kiume na dawa za wagonjwa wa figo. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kamati ya Kudhibiti Uuzaji na Usambazaji wa Bidhaa za Matibabu zisizo na viwango na bandia, Waziri wa Afya Aden Duale amesema serikali inaanzisha mfumo wa kitaifa wa kidijitali wa kufuatilia dawa. Mfumo huo unatarajiwa kuwezesha ufuatiliaji wa kila dawa inayosambazwa nchini. Mary Muoki na taarifa hiyo.