Katibu wa wizara ya afya Dkt. Ouma Oluga ametoa wito wa kuimarishwa kwa uratibu kati ya teknolojia ya tiba, biashara na ubunifu ili kusaidia kupunguza gharama za huduma za afya na kupanua upatikanaji wa huduma bora.
Olunga alisema kuwa kuleta pamoja teknolojia, biashara na ubunifu ni muhimu katika kutoa huduma za afya zilizo nafuu na zenye ufanisi zaidi. Olunga alizungumza alipofungua rasmi maonesho ya 26 ya matibabu jijini Nairobi. Maonesho ya kimataifa yanayowaleta pamoja wadau wa sekta na wavumbuzi ili kuonesha teknolojia mpya za matibabu.