Skip to main content
Skip to main content

Tetemeko Afghanstan: Zaidi ya watu 800 wahofiwa kufariki

  • | BBC Swahili
    4,368 views
    Duration: 54s
    Serikali ya Taliban nchini Afghanistan imesema kuwa zaidi ya watu 800 wanahofiwa kufariki kufuatia tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 6.0 lililotokea katika mkoa wa mashariki wa Kunar usiku wa kuamkia Jumatatu. Zaidi ya watu 2,500 wanaaminiwa kuwa wamejeruhiwa. Tetemeko hilo lilitokea karibu na Jalalabad - eneo la mbali na la milima karibu na mpaka wa Pakistan, jambo linalofanya shughuli za uokoaji kuwa ngumu. Jiunge na @HamidaAbubakar kwa haya na mengi kwenye Dira ya Dunia TV mubashara saa tatu usiku kupitia ukurasa wa YouTube BBC Swahili. Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw