Kwa watu wengi wanaoishi na ugonjwa wa vitiligo, changamoto zao ni nyingi wala sio tu mabadiliko ya rangi ya ngozi. Wengi wao hukabiliana na miaka mingi ya unyanyapaa, dhihaka na kukosa hadhi, huku wakijaribu kuishi katika jamii ambayo mara nyingi hauelewi ugonjwa huo. Hata hivyo, katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Vitiligo, kuna matumaini mapya baada ya watafiti katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta kuanza majaribio ya hatua ya tatu ya tiba mpya. Tiba hiyo inaweza kusaidia kurejesha rangi ya ngozi na kubadilisha maisha ya maelfu ya watu wanaoishi na vitiligo