Timu hizo 12 zilijinyakulia ubingwa wa kaunti zao baada ya kushinda fainali za kaunti.
Huko Kisumu, Obunga FC iliichapa Julu Nyambugu 4-1 kwa mikwaju ya penalti baada ya mechi kumalizika kwa sare tasa. Mabingwa watetezi mara mbili, Nyakach Girls, walihifadhi taji lao la kaunti kwa kuifunga Victoria Soccer Academy 4-0.
Huko Siaya, Indomitable Soldiers waliifunga Real Talent Academy 10-9 kwa mikwaju ya penalti baada ya mchezo kumalizika 1-1 katika muda wa kawaida. Katika kitengo cha wasichana, Nyamira Starlets waliwashinda Lwak Starlets 6-5 pia kwa mikwaju ya penalti.
Wawakilishi wa Migori ni Awendo Academy na Oyugi Ogango Girls.