Timu 44 zitashiriki katika michuano ya Rashid Abdalla Super Cup makala ya saba baada ya droo ya mashindano hayo kufanyika katika ukumbi wa Kwale Culture mjini Kwale.
Timu hizo zimepangwa katika makundi 11, ambapo kila kundi litakuwa na timu nne zitakazoshindana katika hatua ya makundi.
Washiriki wa mashindano hayo wanatoka kaunti za Kwale, Mombasa, Tana River na Kilifi huku waandalizi wakisema wachezaji wote hawatazidi umri wa miaka 25 ikiwa ni sehemu ya juhudi za kukuza vipaji vya vijana.
Mechi hizo zinatarajiwa kuanza tarehe 11 Julai huku fainali ikipangwa kuchezwa tarehe 20 Disemba mwaka huu.