- 1,641 viewsDuration: 2:26Matokeo ya upasuaji wa mwili wa Margaret Wambui, aliyefariki baada ya kuanguka kutoka kwenye jumba la Altura, mtaani Upper Hill, yameonyesha kuwa alifariki kutokana na majeraha mabaya. Wambui, aliyekuwa na umri wa miaka 21, alivunjika viungo mbalimbali vya mwili, ikiwemo uti wa mgongo. Uchunguzi umebaini kuwa alikuwa kwenye paa la jengo hilo kwa zaidi ya dakika 40 kabla ya kuonekana akianguka.