Skip to main content
Skip to main content

Ufadhili wa michezo ya wanafunzu wenye mahitaji maalum

  • | Citizen TV
    1,003 views
    Duration: 3:04
    Serikali imetakiwa kutenga fedha za kusaidia shughuli za michezo miongoni kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum. Wadau wa elimu na michezo wanasema wanafunzi hawa wana vipaji mbalimbali vya michezo, lakini ukosefu wa ufadhili umekuwa ukiwazuia kushiriki kikamilifu katika mashindano. Wakizungumza katika Shule ya Cheribisi Integrated wakati wa hafla ya kuwapokea wanafunzi wawili wenye mahitaji maalum waliowakilisha Kenya katika Michezo ya Shule Maalum ya Afrika Mashariki iliyokamilika hivi majuzi, wadau hao walisema michezo ni nyenzo muhimu ya kukuza vipaji na kujiamini miongoni mwa wanafunzi wenye ulemavu.