Serikali inasema inaongeza juhudi kukabiliana na uhaba wa maziwa unaoshuhudiwa nchini, hali inayochangiwa zaidi na ukame wa muda mrefu na kupanda kwa gharama ya chakula cha mifugo. Wizara ya Kilimo inasema uzalishaji wa maziwa ulipungua kwa takriban asilimia 3.7 mwezi Julai, huku hali ikitarajiwa kuimarika baada ya mvua kurejea na malisho kuota. Serikali inapanga kuwezesha uagizaji wa tani 500,000 za mahindi ya manjano bila ushuru, kwa ajili ya kutengeneza chakula cha mifugo, huku ikitafuta hifadhi zilizopo za chakula cha mifugo ili kukabiliana na uhaba