- 205 viewsDuration: 1:56Uharibifu wa makazi ya wanyama pori umetajwa kama chanzo kikubwa cha migogoro baina ya wanyama na binadamu nchini. Katibu wa uhifadhi katika idara ya wanyama pori Dkt. John Kipkorir Chumo amesema kuongezaka kwa idadi ya watu kumechangia uharibifu wa mazingira na kusababisha wanyama kuingia maeneo ya makazi ya binadamu hali inayohatarisha maisha yao.