- 25,426 viewsDuration: 3:10Rais mstaafu Uhuru Kenyatta amewaonya wakazi wa Mlima Kenya dhidi ya kile amesema ni kutorudia makosa waliofanya kwenye uchaguzi mkuu uliopita. Rais mstaafu akiwataka wakaazi wa Mlima Kenya kuungana, akiendelea kuwaonya dhidi ya wanasiasa wenye maneno matamu. Uhuru, aliyehudhuria mazishi Kirinyaga, pia amewaonya viongozi wa makanisa dhidi ya kuingilia maswala ya siasa, akiwalaumu kwa kuwapotosha wakazi wa Mlima Kenya kwenye uchaguzi uliopita.