Mamlaka ya udhibiti wa miradi ya maji nchini imedokeza kuwa asilimia 80 ya ujenzi wa bwawa la mwache kaunti kwale umekamilika na kuwa mradi huo utatatua changamotoo ya maji hasa katika kaunti ya Mombasa.
Wakizungumza huko Mombasa wakati wa kongamano na wajumbe katika sekta ya maji nchini pamoja n kutoa hundi ya shilingi milioni 49 kwa makundi 10 ya kuhifadhi mazingira karibu na bwawa hilo , mwenyekiti wa mamlaka hiyo Donald Murgor, na afisa mkuu mtendaji Mohamed Shurie wametaka makundi hayo kubuni miradi inayowawezesha kujitegemea .