Ujenzi Wa Uwanja Wa Kamariny Katika Kaunti Ya Elgeyo Marakwet Unaotarajiwa Kuandaa Sherehe Za Mashujaa inatarajiwa Kukamilika katika Ndani Ya Miezi Mitano Ijayo. Haya Ni Kwa Mujibu Wa Mkurugenzi Mkuu Wa Sports Kenya Timothy Kilimo.
Akizungumza Baada Ya Kuzuru Uwanja Huo Kukagua Maendeleo Ya Ujenzi, Kilimo Amesema Serikali Imejizatiti Kuhakikisha Maandalizi Yote Yanakamilika Kwa Wakati Uliowekwa. Mbunge Wa Keiyo Kaskazini Adams Kipsanai Amewataka Wakazi Kuepuka Kuingiza Siasa Katika Mradi Huo, Akisema Serikali Imeweka Mikakati Madhubuti Kuhakikisha Uwanja Huo Unafikia Viwango Vya Kimataifa.