- 607 viewsDuration: 2:45Wakulima wa mahindi katika Kaunti ya Trans Nzoia wamegubikwa na hofu baada ya mimea yao shambani kuanza kunyauka kutokana na ukosefu wa mvua. Tathmini ya awali ya wizara ya Kilimo imebaini kuwa kati ya ekari laki mbili unusu zilizopandwa mahindi, zaidi ya ekari elfu hamsini tayari zimeathirika vibaya .