Skip to main content
Skip to main content

Upinzani wadai Bandari ya Mombasa imebinafsishwa

  • | Citizen TV
    3,592 views
    Duration: 2:38
    Viongozi wa upinzani wanadai kuwa Bandari ya Mombasa imebinafsishwa, wakipinga hatua hiyo na kutaka uwazi katika usimamizi wa mali ya umma. Kinara wa Wiper, Kalonzo Musyoka, akishirikiana na viongozi wengine wa upinzani, akiwemo Justin Muturi wa DP na Eugene Wamalwa wa DAP-K, wamesema hawatakubali ubinafsishaji wa mali ya umma bila kufuatwa kwa sheria. Pia wametaka kuwepo kwa uwazi katika utekelezaji wa miradi ya serikali, ikiwemo ujenzi wa kiwanda cha mafuta cha Lamu.