Skip to main content
Skip to main content

Upinzani wadai njama fiche kuelekea uchaguzi mdogo wa Ol Kalou

  • | Citizen TV
    7,554 views
    Duration: 3:11
    Viongozi wa upinzani sasa wanadai kuna njama fiche baada ya Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja kutangaza kutumwa kwa zaidi ya maafisa 1,000 wa polisi kuimarisha usalama katika eneo bunge la Ol Kalou wakati wa uchaguzi mdogo wa Alhamisi. Wakiongozwa na Kalonzo Musyoka na Martha Karua, viongozi hao wameendelea kuilaumu Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kwa kile wanachodai ni kufumbia macho matukio ya uhuni yaliyoshuhudiwa wakati wa kampeni za uchaguzi huo mdogo.