- 1,472 viewsDuration: 1:52Viongozi wa upinzani wamelaumu vikali tume ya uchaguzi IEBC kwa madai ya kukosa kuwaita kujadili maswala tata yaliyoibuliwa kwenye maandalizi ya uchaguzi wakisema tume hiyo inazidi kupuuza masuala wanayoibua. Wakizungumza kule Kibwezi East, Makueni katika hafla ya mazishi ya marehemu Jaji Joseph Mbalu, viongozi hao wamesema hawatasalia kimya huku Rais William Ruto akiendelea kukiuka katiba, haswa kukandamiza wananchi, utekaji nyara na kuwafurushwa wawekezaji. Haya ni huku kiongozi wa People's Party Ndindi Nyoro naye akikita kambi maeneo ya Ruiru Kaunti ya Kiambu kurindima siasa ya Wantam.