- 9,637 viewsDuration: 2:37Vinara wa upinzani wamemtaka Rais William Ruto kukoma kumshambulia mtangulizi wake, Rais mstaafu Uhuru Kenyatta, wakitaja madai ya Rais ya Alhamisi kuwa jaribio la kukwepa kuwajibishwa. Wakiongozwa na kinara wa DCP Rigathi Gachagua, aliyezuru Kaunti ya Nakuru Ijumaa, vigogo hao wamemtaka Rais Ruto kujiandaa kubwagwa debeni mwaka ujao, wakidai Wakenya hawana lolote la kusherehekea katika utawala wake. Kama anavyoarifu Kamau Mwangi, wenzake Kalonzo Musyoka na Fred Matiang’i walizungumza walipozuru Malindi, Bomet na Narok mtawalia.