Skip to main content
Skip to main content

Upinzani wataka Marekani kuheshimu amri ya mahakama kuhusu kituo cha Ebola Nanyuki

  • | Citizen TV
    742 views
    Duration: 1:34
    Viongozi wa upinzani wametaka serikali ya Marekani kuheshimu sheria za Kenya na kutii amri ya mahakama iliyositisha ujenzi wa kituo cha karantini ya Ebola katika eneo la Nanyuki, wakisisitiza kuwa maoni ya Wakenya lazima yazingatiwe. Akizungumza katika Kanisa la A.I.C Karen, viongozi hao pia wamelitaka Kanisa kutoa msimamo na mwongozo kuhusu uongozi bora unaofaa nchini, wakisema taasisi za kidini zina jukumu muhimu katika kuimarisha uwajibikaji na maadili ya uongozi. Wamesema ni muhimu kwa miradi ya kimataifa inayotekelezwa nchini kuendana na sheria za ndani na kuheshimu maamuzi ya mahakama.