Jaji wa mahakama ya rufani, Kipchumba Katwa Kigen, amejitetea kuwania nafasi ya kuwa kwenye jopo la majaji saba wa mahakama ya upeo akisema kuwa uwakilishi wake wa kisheria wa rais William Ruto katika mahakama ya kimataifa ICC kwenye kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais wa mwaka 2022 hautaathiri uhuru wake akiwa kwenye jopo hilo. Shughuli ya usaili wa kumtafuta mrithi wa marehemu Jaji Mohamed Khadhar Ibrahim pia ilijumuisha aliyekuwa mwenyekiti wa halmashauri ya kutathmini utendakazi wa polisi IPOA, Anne Makori, pamoja na Jaji Joseph Kiplagat Sergon wakijivunia uzoefu wao mpana katika masuala ya katiba, sheria na uongozi wa taasisi. Mwanahabari wetu Ruth Wamboi anatuletea taarifa hiyo.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive