- 2,377 viewsDuration: 2:41Maafisa wa usalama walikesha wakidhibiti hali ya usalama katika eneo la Githurai 45 huku barabara kuu ya Thika ikifungwa kwa saa nyingi. Polisi katika eneo hilo walilazimika kuwakabili vijana waliodaiwa kujaribu kuwapora wananchi wakati wa shughuli za siku. Maafisa wa vitengo maalum vya polisi walishiriki doria katika sehemu kubwa ya Githurai ili kuimarisha usalama na kudhibiti hali.