- 3,724 viewsDuration: 3:27Maafisa wa usalama walifunga barabara nyingi za kuingia na kutoka jijini Nairobi huku wakiimarisha doria katika maeneo mbalimbali. Kuanzia barabara ya Thika hadi Waiyaki na hata ile ya Mombasa, nyaya za kufunga barabara zilionekana katika sehemu nyingi huku magari na wasafiri wakikabiliwa na usumbufu wa muda. Hatua hizo zilichukuliwa wakati shughuli za siku zikiendelea katika jiji hilo. Gatete Njoroge anaangazia namna usalama ulivyodhibitiwa katika maeneo mengi ya kuingia na kutoka jijini Nairobi.