- 4,166 viewsDuration: 2:42Maelezo zaidi yanaibuka kuhusu makubaliano yaliyotiwa saini kati ya Kenya na Marekani ambayo sasa yamezua utata kuhusu mpango wa kuanzishwa kwa kituo cha karantini ya Ebola katika eneo la Laikipia. Taarifa kuhusu mkataba huo wa kisheria wa ushirikiano wa kupunguza vitisho vya kibayolojia zinaonyesha kuwa serikali ya Marekani ilipewa mamlaka makubwa ya kusimamia na kuelekeza miradi inayotekelezwa chini ya makubaliano hayo. Haya yanajiri huku visa vya Ebola vikiendelea kuongezeka katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), hali inayoongeza mjadala kuhusu usalama wa afya ya umma na ushirikiano wa kimataifa katika kukabiliana na milipuko ya magonjwa. Mwanahabari Brenda Wanga anaripoti kwa kina kuhusu vipengele vya mkataba huo na mjadala unaoendelea.