Vijana katika Trans Nzoia wameanzisha mpango wa kutoa hamasisho kuhusu jinsi ya kukabiliana na visa vya wanasiasa kuwatumia kama wahuni. Badala yake Vijana wakihimizwa kutumia vipaji vyao kujikimu kimaisha.
Wakizungumza baada ya mechi ya soka ya jamii katika Uwanja wa Ndura, viongozi na wadau katika eneo hilo walisisitiza umuhimu wa kuwekeza katika kukuza vipaji, mafunzo ya ujuzi, na ujasiriamali. Walisema ushirikiano kati ya serikali, sekta binafsi, na asasi za kiraia unaweza kusaidia vijana na wanawake kujitegemea na kuchochea ukuaji wa uchumi endelevu. Aidha Wanaiomba serikali kuongeza ufadhili kwa mipango ya kuunda nafasi za ajira kwa vijana ili kupunguza wao kutumia kuzua vurugu katika mikutano ya kisiasa.