Kufuatia ongezeko la idadi ya wakongwe wanaohitaji huduma za uangalizi uzeeni, vijana wanaojiunga na vyuo vya kiufundi wametakiwa kujisajili kwa kozi ya huduma kwa wakongwe ili kusaidia kuziba pengo la wahudumu wanaohitajika.
Wito huo umetolewa katika hafla ya pili ya kufuzu kwa wahudumu ishirini na mmoja wa Chuo cha Mafunzo ya Afya cha Steps iliyofanyika Ruiru, kaunti ya Kiambu.
Wadau wanasema mafunzo hayo yanaweza kusaidia kukidhi mahitaji yanayoongezeka ya huduma kwa wazee na kufungua nafasi zaidi za ajira kwa vijana. Kamau Mwangi anaripoti.