Skip to main content
Skip to main content

Vijana wailaumu serikali kwa kuwatenga katika maamuzi

  • | Citizen TV
    692 views
    Duration: 3:19
    Baadhi ya vijana sasa wanailaumu serikali kwa kuwatelekeza, wakipinga madai kwamba wamepoteza maadili na kutumiwa vibaya na wanasiasa kusababisha machafuko na uhuni. Vijana waliohudhuria kongamano la Kanisa Katoliki hapa Nairobi waliilaumu serikali kwa kutowashirikisha katika maamuzi, wakitaja hali hiyo kama sababu inayowafanya baadhi yao kutumiwa kisiasa. Kanisa Katoliki, kwa upande wake, limekiri kuwa halijawahusisha vijana ipasavyo na kuahidi kushinikiza serikali kuwajumuisha katika kila hatua ya maamuzi ili kupunguza migogoro ya mara kwa mara kati yao na serikali.