- 2,486 viewsDuration: 2:48Viongozi wa kisiasa na kidini katika Kaunti ya Turkana wamelalamikia ongezeko la mashambulizi yanayohusishwa na wezi wa mifugo. Watu watatu wameuawa na mifugo kuibwa, huku mifugo hiyo ikiwa bado haijapatikana. Viongozi hao sasa wametishia kusitisha shughuli za uchimbaji mafuta hadi serikali itakapowarejeshea mifugo iliyoibwa na kufidia familia zilizopoteza wapendwa wao.