- 60 viewsViongozi wa jamii mbalimbali kutoka Bangale wanaitaka idara ya usalama kuanzisha msako wa silaha haramu kufuatia kurejea kwa mapigano ya kijamii katika eneo hilo. Viongozi hao wanasema hatua hiyo itasaidia kurejesha amani, kuimarisha usalama wa wananchi na kuzuia kuendelea kwa machafuko yanayotishia maisha na mali ya wakazi.