- 366 viewsDuration: 2:29Viongozi wa mataifa mbalimbali jioni hii wanatazamiwa kutoa taarifa ya pamoja kuhusu maazimio yao baada ya kukamilika kwa kongamano la Africa Forward jijini Nairobi. Kenya na Ufaransa zimekuwa wenyeji wa kongamano hilo kupitia Marais William Ruto na Emmanuel Macron. Kongamano hilo liliangazia sekta muhimu kama kawi, uchumi wa baharini, teknolojia, kilimo endelevu, afya, mikopo, amani, usalama na masuala ya vijana.