- 250 viewsDuration: 3:30Kanisa Katoliki katika mji wa Kitengela, Kaunti ya Kajiado kwa ushirikiano na wafadahili wengine, latarajiwa kutumia makala ya tatu ya Mbio za Kijamii kuhubiri umoja, amani na mshikamano miongoni mwa vijana. Viongozi wa kanisa hilo wasema Kitengela imekuwa kitovu cha machafuko kila kunapotokea maandamano, na kuwa ni wakati wa kutafuta njia za kuwafikia vijana kwa mazungumzo kupitia jukwa la michezo.